MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya ameviagiza vyombo ambavyo havijaanza kuchangia huduma za maji vianze mara moja kuchangia ili huduma ya maji iwe endelevu.
Malenya ametoa agizo hilo katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Namtumbo Fransis Mgoloka kwenye kikao Cha vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya Jamii kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo .
Mkuu wa Wilaya pia amemwagiza Meneja Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini(RUWASA) Wilaya ya Namtumbo kusimamia Kwa dhati utekelezaji wa sheria namba 5 ya mwaka 2019 inayotaka kuunda Jumuiya ya watumia maji ili kuchangia huduma ya maji .
Pamoja na hayo aliagiza ofisi ya bonde za ziwa Nyasa na mto Ruvuma zihakikishe vyombo vya watumia maji vinakuwa na vibali vya kutumia maji huku akiwaagiza RUWASA kuendelea na zoezi la kuunda kamati zilizobaki katika vijiji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.