• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DC SONGEA azindua miongozo mitatu ya Elimu

Imewekwa kuanzia tarehe: December 7th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa pololet Mgema  amezindua miongozo mitatu ya usimamizi na uendeshaji wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Hafla ya uzinduzi huo imehudhuriwa na wadau wa elimu kutoka  Manispaa ya Songea na kufanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Songea Girls mjini Songea.

Akizungumza kabla ya kuzindua miongozo hiyo Mkuu wa Wilaya  amesema uzinduzi huo wa miongozo ya elimu ni muendelezo wa utekelezaji wa uzinduzi wa kitaifa uliofanywa na Waziri Mkuu  na uzinduzi wa  kimkoa uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Amesema ili miongozo hiyo iweze kuleta ufanisi,inafaa ieleweke vizuri kwa wadau wote wa elimu katika ngazi ya shule na ngazi ya jamii na kwamba miongozo imeanisha masuala mbalimbali ya elimu ikiwemo changamoto za kielimu na  utatuzi wake katika shule za msingi na sekondari.

“Changamoto kubwa zinazotakiwa kufanyiwa kazi ni udhibiti wa utoro wa wanafunzi,Mkuu wa shule ahakikisha wanafunzi wanaitwa majina mara mbili kwa siku ili kujua kama kuna watoro ,pia  mzazi aitwe shuleni iwapo mtoto wake hatahudhuria shule siku mbili mfululizo’’,alisisitiza.

Mkuu wa wilaya pia amewaagiza wadau wa elimu kutafutia ufumbuzi changamoto ya ukosefu wa chakula shuleni,amemwagiza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea,kuangalia uwezekano wa kutunga sheria zinazowabana wazazi ambao hawataki kuchangia chakula kwa Watoto wao na kwamba agenda ya chakula iwe ya kudumu kwenye vikao.

Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya pia aliagiza wadau wa elimu kutafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu,ikiwemo upungufu wa samani,vyoo,vyumba vya madarasa, upungufu wa walimu na kutoa mafunzo kazini kwa walimu.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Alto Liwolelu aliitaja miongozo mitatu ambayo imezinduliwa kuwa ni  Mwongozo ambao umeainisha changamoto katika elimu ya msingi na sekondari.

Ameutaja mwongozo wa pili kuwa  unahusu mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya elimu ya msingi na mwongozo wa tatu umeeleza kuhusu uteuzi wa  viongozi wa elimu katika mamlaka za serikali za  mitaa na mikoa.

Hata hivyo amesema miongozo yote mitatu imebeba changamoto na taratibu za usimamizi na uendeshaji wa elimu ya msingi na sekondari na kwamba miongozo hiyo inakusudia kuleta tija katika sekta ya elimu kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano amewaagiza walimu wakuu kuhakikisha katika shule zao wanapanda miti ikiwemo miti ya matunda ili kuhifadhi mazingira katika shule zao.

Kuhusu upatikanaji wa chakula shuleni,Mbano amesema watafanya mikutano na wazazi ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuchangia chakula kwa Watoto wao wanapokuwa shuleni.

Naye Afisa Elimu Shule za Msingi Katika Manispaa ya Songea Frank Sichalwe akizungumzia kwa ujumla changamoto za walimu,amekiri kwenye Halmashauri za Manispaa,miji na majiji hakuna mwalimu anayehamia,pia katika Halmashauri hizo hakuna ajira mpya za walimu.

“Tuna uhaba mkubwa wa walimu,wakati huo huo walimu walio wengi wanastaafu kwa hiyo katika  Manispaa ya Songea hakuna shule hata moja yenye mwalimu wa ziada’’,alisisitiza Sichalwe.

Kuhusu upatikanaji wa miundombinu katika shule za msingi,Sichalwe amesema anaishukuru serikali  ambayo hivi sasa inajenga madarasa mengi katika shule za msingi hivyo kupunguza uhaba wa miundombinu ya madarasa katika manispaa ya Songea.

Hata hivyo amesema baada ya serikali kutoa miongozi hiyo mitatu ya elimu,Manispaa ya Songea inakwenda kutafutia ufumbuzi changamoto hiyo ya uhaba wa walimu na changamoto nyingine ili kuboresha elimu ya msingi na sekondari.

Miongozo hiyo mitatu ya usimamizi wa elimu imeundwa Julai mwaka huu kupitia Wizara ya TAMISEMI ikiwa ni juhudi za serikali ya awamu ya sita kuboresha elimu ili wananchi wake wapate elimu bora na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Tanzania.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ruvuma

Novemba 7,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.