Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma MheJulius Mtatiro, amekagua miundombinu ya maji na vyoo katika sekondari ya Ligunga.
Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Mtatiro amebaini uchakavu wa vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi na vyoo vya walimu pamoja na shida ya maji.
Mkuu wa wilaya ameagiza ujenzi wa dharura wa vyoo hivyo uanze mara moja ili kumaliza kero hiyo.
“Ninaagiza ujenzi wa dharura wa vyoo vya shule hii uanze mara moja vyoo hivi ni muhimu kwa wanafunzi na walimu, na ni lazima viwe katika hali nzuri.”,alisisitiza Mtatiro.
Mtatiro amemwagiza Meneja wa Usambazaji Maji Vijiji (RUWASA), Eng. Maua Lugala, kuhakikisha wanashirikiana na TANESCO ili kufanya tathmini ya kuweza kusogeza maji karibu zaidi na shule hiyo.
Meneja wa TANESCO Tunduru na Meneja wa RUWASA wameahidi kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha Shule ya Sekondari Ligunga inakuwa na maji ya uhakika .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.