Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe.Wakili.Julius Mtatiro amehimiza watoto kuandikishwa shuleni, na kusisitiza kuwa elimu ni msingi wa mustakabali wa watoto na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Amesema watoto wanaopata elimu wanakuwa na uwezo mkubwa wa kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwa raia mwema katika jamii. Pia, asisitiza kuwa elimu ni njia ya kupambana na ujinga na umaskini ili kuwezesha maendeleo endelevu katika Wilaya yetu.
“Serikali inatoa fedha nyingi ili kuboresha miundombinu ya shule, kutoa vifaa vya kufundishia pamoja na kujifunzia” alisema Mhe.Wakili Mtatiro “Ni jukumu letu sote kuhakikisha watoto wanaandikishwa ili wapate elimu bora”,alisema Mtatiro
Aidha, Mhe.Wakili Mtatiro awahimiza wazazi kuchukua jukumu la kuwaandikisha watoto wao shuleni na amewakumbusha wazazi kuwa elimu ni haki ya kila mtoto na ni jukumu lao kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu bora.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.