• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DC Tunduru anavyotekeleza maagizo ya RC Ruvuma,ng'ombe 800 wakamatwa

Imewekwa kuanzia tarehe: July 14th, 2023

MKUU wa wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro anaendelea kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ya kuwaondoa wafugaji holela ambapo  amesema,wamekamata zaidi ya ng’omba 800 waliovamia mashamba na kuharibu mazao ya wakulima katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Amesema,ng’ombe hao wamekamatwa kutokana na  doria na operesheni kubwa inayoendelea ya kuwaondoa wafugaji  wote wanaofanya shughuli za ufugaji na kuingiza mifugo kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kisheria.

Mtatiro amesema hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake,na kusisitiza kuwa ni lazima wafugaji wote kwenda katika maeneo(vitalu)vilivyotengwa kwa ajili  kufugia mifugo badala ya kuendelea na ufugaji holela.

“kuna tabia ya baadhi ya wafugaji kupeleka kwa makusudi mifugo yao kwenye mashamba na kuharibu mazao  ya wakulima jambo linalosababisha migogoro mikubwa kati ya wakulima na wafugaji hao”alisema.

Kwa mujibu wa Mtatiro,serikali itaendelea kufanya doria na operesheni ya kuwaondoa wafugaji wote waliovamia kwenye maeneo yasiyoruhusiwa na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vikosi vinavyofanya kazi ya kuondoa mifugo katika vijiji vyao.

Alisema,mwaka 2019 serikali wilayani Tunduru ilitenga jumla ya vitalu 250 ili vitumike kwa ajili ya ufugaji,hata hivyo ni vitalu 125 tu vimelipiwa na kutumika kwa ajili ya kazi hiyo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya alisema,wamemkamata Afisa mtendaji wa kijiji cha  Machemba na Misechela na wenyeviti wa vijiji hivyo,kwa  kuruhusu wafugaji kuingiza mifugo kwenye maeneo ambayo hayakutengwa kwa ajili ya ufugaji.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Namasakata wilayani humo wamesema,kata hiyo hakuna vitalu vya mifugo vilivyotengwa kwa ajili ya ufugaji, lakini kuna makundi makubwa ya mifugo.Diwani wa kata hiyo Rashid Usanje alisema,makundi ya mifugo yanavamia mashamba na kuharibu mazao mashambani na kuiomba Serikali kuchukua hatua kuwadhibiti wafugaji na mifugo yao.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.