Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mheshimiwa Simon Chacha amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Misechela na kata ya Namasakata,lengo kubwa lilikuwa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya aliwaonya wafugaji holela wanaokaidi agizo la kupeleka mifugo yao kwenye vitalu vilivyotengwa ambapo amewaagiza waache kupeleka mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima na badala yake wafuate sheria kwa kuweka mifugo yao kwenye vitalu.
Mkuu wa Wilaya pia aliwaasa wakulima na wafugaji kukaa pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto zao kwa amani badala ya migogoro.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.