• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DC TUNDURU ataka kasi ya upandaji miti kulinda mazingira

Imewekwa kuanzia tarehe: November 1st, 2022

MKUU wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro amesema,ni muhimu suala la upandaji miti katika wilaya hiyo liwe endelevu na jambo la mara kwa mara ili kusaidia uhifadhi wa mazingira.

Mtatiro amesema hayo,baada ya kuongoza zoezi la upandaji  miti lililofanyika katika eneo la Kanisa la Upendo la Kristo Masihi (KIUMA) kata ya Matemanga wilayani humo.

Mtatiro,amewakumbusha viongozi wa ngazi za vijiji,kata na Halmashauri  kuendelea kuhamasisha wananchi kupanda miti katika maeneo yao na kushauri aina ya miti inayofaa ambayo haina athari kimazingira hasa kwenye vyanzo vya maji.

Alisema,uharibifu wa mazingira unaongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na shughuli za kibinadanu ikiwamo kilimo na ufugaji holole, huku waharibifu hao wakishindwa kupanda miti mipya katika maeneo hayo,jambo linalo weza kuhatarisha maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.

Alisema,suala la upandaji miti ni muhimu katika jamii yetu kwani itasaidia sana kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa inayoweza kuhatarisha maisha ya Binadamu,hivyo wananchi wana wajibu wa kuzuia hatari  hiyo.

Aidha,amelipongeza kanisa hilo kwa kuandaa zoezi la upandaji miti na kuzitaka taasisi nyingine za dini,serikali na binafsi kuiga mfano wa Kanisa la Upendo kutokana na harakati zake  za kupanda miti mara kwa mara ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Alisema,serikali imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha inatunza mazingira ambapo alitaja miongoni mwa mikakati hiyo ni kupanda miti kwa wingi katika taasisi,idara za serikali na  taasisi binafsi.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini Hassan Kungu alisema,amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji mazingira kwa kupanda miti kwa wingi katika maeneo yao.

Naye Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiuma Daniel Malukuta alisema,kila mwaka taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kuotesha miche na kupanda miti kuzunguka maeneo yake ili kutunza mazingira na kuhamasisha jamii na waumini wa kanisa la Upendo kuona suala la upandaji miti ni muhimu katika maisha yao.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.