• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DC TUNDURU awataka mafundi ujenzi miradi ya serikali kuepuka udanganyifu

Imewekwa kuanzia tarehe: June 1st, 2023

SERIKALI wilayani Tunduru,imewataka mafundi  wanaofanya kazi za ujenzi wa miradi ya maendeleo kuepuka kushirikiana na  watendaji wasiokuwa waaminifu hasa maafisa manunuzi wa Halmashauri kufanya udanganyifu juu ya ubora wa miradi ili kujipatia fedha.

Kauli hiyo imetolewana Mkuu wa wilaya hiyo  Mheshimiwa Julius Mtatiro,baada ya kuzindua ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa ambapo kati ya hivyo,viwili kwa ajili ya elimu ya awali,matunduu ya vyoo,jengo la utawala na kichomea taka katika shule ya msingi Ligoma  wilayani humo.

Madarasa hayo na miundombinu mingine ya elimu, yanajengwa kupitia mradi wa kuboresho  upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora kwa elimu ya awali na msingi(Boost) ambapo serikali imetoa jumla ya Sh.milioni 513,200,000.00.

Aidha Mtatiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo, amewaonya wahandisi kuhakikisha wanatekeleza miradi ya ujenzi kwa kuzingatia sheria za usimamizi wa fedha na manunuzi ya fedha za serikali za mitaa na siyo vinginevyo.

Amewakumbusha kuhusu umuhimu wa mradi huo, na kutothubutu kabisa kubadili matumizi ya fedha kwa kuwa serikali imeshafanya tathimini ya kina kuhusu maeneo  yaliyopangwa kujengwa shule au kufanya ukarabati wa miundombinu katika maeneo yote.

Alisema,kupitia mpango wa Boost Serikali imeweka kipaumbele kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa wanafunzi,vijiji visivyokuwa na shule,maeneo ambayo wanafunzi wake wanatembea umbali mrefu na shule zenye uchakavu.

Mtatiro,amempongeza RaiS Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ubunifu wake wa kutafuta fedha ambazo zinakwenda kuondoa kero za ufundishaji  kwenye shule za msingi wilayani Tunduru.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Chiza Marando,amewaomba wananchi kusaidia ulinzi wa vifaa vya ujenzi pale vinavyotoka stoo hadi eneo la ujenzi  kwani baadhi ya mafundi na wasimamizi wanatumia nafasi hiyo kuiba vifaa vinavyoletwa kwa ajili ya kazi.

Amemuagiza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,kuhakikisha vifaa vyote vinavyotoka stoo vinasindikizwa na wajumbe wa kamati ya ujenzi na kamati ya manunuzi kwani kuna baadhi ya watu wanaweza kukwamisha utekelezaji wa miradi ya Boost.

Amewaomba wananchi wa Ligoma na maeneo mengine ambayo miradi hiyo inatekelezwa,kutoa ushirikiano kwa kamati za ujenzi na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa.

.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.