• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DC TUNDURU kuwafukuza wafugaji wasiokwenda kwenye vitalu

Imewekwa kuanzia tarehe: February 12th, 2023

SERIKALI ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma imesema,itawakamata na kuwatoza faini  kubwa wafugaji  wote wanaoishi kiholela na kuchunga mifugo nje ya maeneo yaliyotengwa(vitalu).

Kauli hiyo imetolewa  na Mkuu wa wilaya hiyo  Mheshimiwa Julius Mtatiro,wakati akizungumza na wafugaji wakati wa ufunguzi wa nyumba ya kulala wageni ya Kajima Guest House iliyojengwa na mfugaji wa jamii ya Kisukuma Mahembo Shamba.

Mfugaji huyo amelazimika kuuza sehemu ya mifugo yake na kujenga nyumba ya kulala wageni, ikiwa ni utekelezaji wa agiza la serikali linalowataka wafugaji kupunguza mifugo na kuwekeza kwenye miradi mingine ya maendeleo.

Aidha Mtatiro alisema,wafugaji watakaochelewa kwenda kwa hiari kwenye vitalu vilivyotengwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kukuta vimejaa wataondolewa kwa nguvu na kupelekwa nje ya mipaka ya wilaya hiyo.

Alisema,hatua hiyo ni maamuzi halali ya serikali katika kumaliza migogoro ya mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima iliyoanza kutokea wilayani humo huku chanzo kikitajwa ni kuwepo kwa baadhi ya wafugaji wasiotaka kufuata sheria na taratibu.

Alisema,katika utekelezaji wa operesheni hiyo,serikali itatumia vikosi vya ulinzi na usalama,ikiwa ni juhudi za kuwaondoa kabisa wafugaji na ufugaji holela unaofanywa na wafugaji wauni katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

“serikali inawapenda wananchi wote wakiwamo wafugaji na ndiyo maana imeandaa utaratibu wa kutenga jumla ya vitalu 279 vyenye ukubwa wa ekari 500 kila kimoja  kwa ajili ya shughuli ya ufugaji”alisema Mtatiro.

Kwa mujibu wa Mtatiro,licha ya mapenzi makubwa ya serikali kwa jamii ya wafugaji wilayani humo,lakini bado kuna  wafugaji  wanakahidi na kufanya ufugaji kiujanja ujanja kwenye makazi ya wakulima na kusababisha migogoro mingi kati ya makundi hayo mawili.

Alisema,wilaya ya Tunduru ni ya kilimo licha ya kukaribisha wafugaji,hata hivyo suruhisho la migogoro inayojitokeza kati ya wakulima na wafugaji ni lazima wafugaji wakapelekwa katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli zao.

Mtatiro,amempongeza mfugaji huyo kwa kuitikia wito wa serikali kwa kupunguza idadi ya mifugo yake na kufanya uwekezaji wa nyumba ya wageni na kuwataka wafugaji wengine kuiga mfano huo.

Kwa upande wake mfugaji huyo alisema,amelazimika kujenga nyumba ya wageni baada ya kupoteza sehemu kubwa ya mifugo yake mkoani Mbeya na Morogoro na amelazimika kuja wilayani Tunduru baada ya kusikia kuna mazingira mazuri  kwa ajili ya kuchungia.

Alisema,hadi kukamilika kwa nyumba hiyo  yenye vyumba 10 vya kulala wageni ametumia fedha nyingi baada ya kuuza Ng’ombe 220 na kuwataka wafugaji wengine kupunguza mifugo yao na kuwekeza katika miradi mingine ya kiuchumi.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.