Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Philemon Magesa ameunda tume ya watumishi watatu kufuatilia madeni yote ya Halmashauri Kwa ajili ya kuanza Kupunguza kulipa .
Magesa alisema Halmashauri lazima iwe na nidhamu ya kupunguza kulipa madeni na ulipaji huo lazima uzingatie umri wa deni husika.
Magesa alisema hayo kwenye kikao kazi kilichowahusisha walimu wakuu ,wakuu wa shule ,watendaji wa kata ,vijiji ,wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo katika ukumbi wa Halmashauri.
Pamoja na hayo aliwataka watumishi kuacha mazoea na kufanya kazi Kwa kujituma na Kwa ufanisi mkubwa katika maeneo Yao ya kazi.
Lengo kuu la kikao hicho lilikuwa kujitambulisha Kwa watumishi ,pamoja na kusisitiza vipaumbele ambavyo ni ukusanyaji mapato, usimamizi wa miradi ya ujenzi pamoja na kuwa na utawala Bora .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.