Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma . Chiza C. Marando, amefanya ziara ya siku mbili kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
Akiwa katika ziara hiyo, ameagiza miradi yote ikamilike na kukabidhiwa ifikapo tarehe 30 Machi 2025 ili wananchi waanze kunufaika nayo.
DED Marando amepongeza jitihada za serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Ameonya kuwa hatosita kuwachukulia hatua wasimamizi wa miradi watakaosababisha ucheleweshaji wa ukamilishaji.
Miradi aliyotembelea ni pamoja na ujenzi wa Zahanati ya Mtangashari, vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Matemanga na Changarawe, matundu ya vyoo katika Shule za Msingi Namwinyu na Matemanga,
Marando pia amekagua ukarabati wa maabara ya kemia katika Shule ya Sekondari Ligunga. Pia, amekagua ujenzi wa mabweni na madarasa katika shule za sekondari Namwinyu na Matemanga.
Katika ziara hiyo, DED Marando amesisitiza kuwa wasimamizi wa miradi, watendaji wa vijiji na mafundi wahakikishe miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyopangwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.