MKOA wa Ruvuma unatajwa kuwa na fursa lukuki za biashara na uwekezaji katika Halmashauri zote nane ambazo zinawawezesha wawekezaji kuwekeza katika shughuli mbalimbali zinazoweza kuchochea ukuaji wa uchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ib uge amezitaja fursa hizo kuwa zipo katika sekta ya kilimo, biashara, ufugaji,utalii,madini,misitu,mawasiliano,umeme wa maporomoko ya maji,uvuvi,viwanda,uendelezaji wa makazi,usafiri na usafirishaji.
Brigedia Jenerali Ibuge amesema katika Mkoa wa Ruvuma kuna maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa viwanda vikubwa,vya kati na vidogo,maeneo ya usambazaji na uuzaji wa bidhaa za viwandani hivyo kuvutia wawekezaji
Kulingana na Mkuu wa Mkoa,maeneo yanayofaa kwa uwekezaji katika sekta kilimo ameyataja kuwa ni usindikaji wa mazao ya chakula hasa mazao ya tangawizi,mafuta,mbogamboga na matunda.
“Serikali imeendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa miundombinu ya barabara na madaraja mkoani Ruvuma inaimarishwa ili kuhakikisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa watu na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuinua uchumi na kupunguza umasikini’’,alisisitiza Ibuge.
Akizungumzia kuhusu meli katika ziwa Nyasa,Brigedia Jenerali Ibuge amesema serikali imenunua meli tatu zinazofanyakazi katika ziwa Nyasa kati hizo meli mbili za mizigo na meli moja ya abiria ambapo meli hizo zinachochea uchumi wa wananchi wanaoishi mwambao mwa ziwa Nyasa na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Kuhusu usafiri wa anga,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema serikali kupitia shirika la Ndege ATCL, imeanzisha safari za ndege mpya mara tatu kwa wiki kati ya Songea na mikoa mingine ya jirani.
Amesema kuimarika kwa safari za anga mkoani Ruvuma kuna fungua fursa za biashara na utalii hivyo kuinua uchumi wa wananchi wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Januari 7,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.