Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imefanya kikao cha tathimini ya Hali ya lishe, kichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kata ya Kilosa mjini Mbambabay.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peres Magiri,aliyewakilishwa na Katibu Tawala ya wilaya ya Nyasa Bw.Salum Ismail amesema kuwa Hali ya Lishe kiwilaya ni nzuri na na hatua zaidi zinazidi kufanyika ili kuimarisha Lishe katika wilaya hiyo..
Akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2014,Afisa Lishe wilaya amesema kuwa watoto wote wanaopatikana na utapiamlo mkali wanapatiwa matibabu na kupona na kwamba Idara mtambuka zinaonesha ushirikiano mzuri katika suala Zima la Lishe ,na watoto wenye umri chini ya miaka mitano walipatiwa matone ya Vitamin A ndani ya Mwezi wa kampeni.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa bw.Pasifiki Mhapa amewataka wajumbe wa kikao hicho kuhakikisha Wanafunzi wote wanapata chakula shuleni ili kudumisha lishe na afya ya wanafunzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.