Utekelezaji wa miradi 15 ya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imepunguza Kwa kiasi kikubwa malalamiko ya upatikanaji wa maji yaliyokuwepo huko nyuma.
Kaimu Meneja wa RUWASA katika wilaya ya Namtumbo Mhandisi Salumu Nachundu amesema kero za upatikanaji wa maji zimepungua baada ya kutekeleza miradi mingi ya maji na kuwawezesha wananchi kupata mahitaji ya maji katika maeneo Yao.
Nachundu amebainisha kuwa utekelezaji wa miradi 15 ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo imepunguza kero za upatikanaji wa maji Kwa wananchi.
Katika utekelezaji wa miradi hiyo Nachundu amesema ipo miradi ambayo imekamilika na kwamba kuna miradi imefika asilimia 65 na miradi mingine ipo katika hatua za awali za kuanza.
Hassan Ndomondo mkazi wa Kijiji Cha Mgombasi kata ya Mgombasiamesema kero ya upatikanaji wa maji katika Kijiji hicho imepungua kutokana na serikali kutoa kiasi Cha shilingi 150,000,000 ili kusambaza maji katika Kijiji hicho na vijiji vya jirani vya Mtumbatimaji na Nangero.
Hali ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Namtumbo Imeongezeka kutoka asilimia 65 hadi kufikia asilimia 71 .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.