HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba msimu wa kilimo 2020/2021 imejipanga kuzalisha mahindi na Maharage tani 146,860 ikiwa msimu wa mwaka 2019/2020 walizalisha zaidi ya tani 113,491
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Joseph Mrimi amesema kuwa katika msimu wa mwaka 2019/2020 Mbolea ilipatikana ilikuwa ni tani 2696.92 na kwamba upatikanaji wa vifuatilifu ulikuwa ni wa lkutosha kwa msimu wa 2019/2020.
“msimu wa kilimo 2020/2021 wanatarajia kuwa na mashamba darasa 17 ili kuwasaidia wakulima kitaalamu,tumeandaa mashamba darasa kitaalamu kwa wakulima wa mfano na wakulima watajifunza hatua kwa hatua juu ya kilimo bora”,alisisitiza.
Hata hivyo Afisa Kilimo huyo amesema mashamba darasa yanaleta tija kwa wakulima na wataalamu ambayo yameandaliwa kwa lengo la kutoa mafunzo juu ya kanuni za kilimo bora cha mazao mbalimbali .
Mrimi ameitaja changamoto ya ukosefu wa vyombo vya usafiri ili kuweza kuwafikia wakulima kwa urahisi katika ngazi ya kata na vijiji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Novemba 16/2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.