Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoa wa Ruvuma inamaeneo mazuri yenye rutuba kwaajili ya kilimo cha mazao ya Biashara na Chakula ikiwemo zao la Palachichi.
Hayo yamesemwa na Afisa kilimo Umwagiliaji na ushirika (W) zao la Palachichi linalolimwa Halamashauri ya Wilaya ya Madaba huzalisha Tani 281.8 katika eneo la Hekta 192.5.
Mrimi amesema zao hilo linalolimwa kata ya Mhanje,Lituta,Mateteleka,Wino na Mkongotema na uzalishaji wake ni mchache hivyo wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika maeneo ya Halmashauri hiyo ili kuongeza uzalishaji kwa wingi na ardhi ya Madaba ni nzuri kwa kilimo ya zao hilo.
“Wananchi wanamwitikio mkubwa kulima zao hilo na wawekezaji waliopo Silverlands Ndolela Ltd ana hekta 95,Kampuni ya Interfruit na inaendelea kulima zao hilo hekta 1200,Shirika la masister st Getrude kijiji cha Ndelenyuma wamepanda jumla ya heka 40 na wakulima wadogo jumla ya heka 59”. Amesema Mrimi.
Hata hivyo Mrimi amesema zao la Palachichi linastawi katika eneo kubwa la Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kutokana na hali nzuri ya hewa na udongo wenye rutuba ya kutosha.
‘’Uzalisha wa Zao la Pala chichi eneo la Halmashauri kwa sasa ni mdogo na tunategemea soko la ndani kwa kiasi kikubwa na kiasi kidogo huuza nje ya Halmashauri”.
Amesema miongoni mwa juhudi wanazoendelea kukuza uzalishaji wa zao hilo Halmashauri inashirikiana na Taasisi ya Tanzanice,Proganic Tanzania LTD,Ofisi ya Maendeleo Jimbo Katoliki la Njombe,Interfruit,Slverlands Ndolela ltd,Shirika la Masister st Getrude Ndelenyuma na wakulima wadogo.
Mrimi amesema zao hilo linakabiliwa kuzalishwa kwa uchache kwa sababu hakuna wawekezaji wengi kutoka sehemu zingine isipokuwa ni wenyeji wa Halmashauri hiyo hivyo husababisha uzalishaji kuwa mdogo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Desemba 1,2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.