HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma,imefanya tathimini ya maendeleo ya Elimu na kufanya vizuri miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2018 hadi 2020 katika matokeo ya elimu ya sekondari mkoani Ruvuma.
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amesema katika Halmashauri zote nane zilizopo mkoani Ruvuma,Halmashauri ya Madaba imeshika nafasi ya kwanza katika mtihani wa kidato cha nne na kwamba Mkutano huo wa tathmini umelenga kuongeza mikakati ya kufanikiwa zaidi katika sekta ya Elimu.
“Tunapozungumzia tathmini ya Elimu tunawagusa moja kwa moja walimu,maswala mengine tunapoona tumekwama moja kwa moja hili swala linakuwa la walimu wametukwamisha na tukifanikiwa tunasahau kusema tumefanikiwa kwa sababu ya walimu tunaomba mtuvumilie”.
Mkuu wa Wilaya amewaomba walimu kuwa huru kuzungumza changamoto zao mambo yaliyopelekea kufanya vizuri na yaliyokwamisha kutofa fanyika vizuri katika sekta ya Elimu.
Mgema ametoa rai kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo kutoa changamoto zinazozikabili shule ambazo zipo kwenye kata zao ili ziwekewe mikakati ya kuzitatua hatimaye kufanya vizuri zaidi.
“Tunatambua uwepo wa wadau wengine kama mchango wa bank yaNMB katika Halmashauri ya Madaba wametuchangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya Elimu,pia TFS nao wametuchangia kwa kiasi kikubwa sana kama mabati,saruji tunaomba muendelee kusukuma gurudumu la Elimu katika halmashauri yetu ya Mdaba’’.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Kassim Mpenda katika kikao hicho amesema mbinu zinazotumika katika kuhakikisha wanafunzi wanadhulia masomo yao vizuri na kufanya zizuri darasani wameweka utaratibu wa kuwatumia watendaji,waratibu wa elimu kata katika ufuatiliaji.
Hata hivyo Mpenda amesema pia wameweka mkakati wakufanya mitihani ya muhula na nusu muhula na pale tu wanapofungua shule wanafanya mitihani iliyopelekea Halmashauri hiyo kufanya vizuri.
“ Tumeimarisha utawala bora shuleni tumekuwa na vikao vya mara kwa mara na walimu wakuu bodi za shule na vikao vya wazazi na kazi hiyo ni endelevu hata kwa walimu wanaokiuka tunawasikiliza kabla ya kuwachukulia hatua, na kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira rafiki japo siyo rafiki kwa asilimia mia moja”.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Orap Pili amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi na walimu wote kwa kazi nzuri wanayofanya na kufikia kuongoza kwa miaka mitatu mfululizo na kupata heshima kubwa katika Halmashauri ya Madaba.
Aidha Makamu Mwenyekiti ameendelea kuwaomba walimu wa Halmashauri hiyo kuwa wavumilimu kutokana na changamoto zinazojitokeza katika mazingira magumu,kwa niaba ya Madiwani amewaahidi walimu kushirikiana katika maeneo ya kazi katika kata na kufuatilia maazimia yaliyowekwa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
April 12,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.