• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HALMASHAURI ya Nyasa yakusanya mapato kwa asilimia 124

Imewekwa kuanzia tarehe: August 27th, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imevuka lengo la ukusanyaji mapato,baada ya kufanikiwa kukusanya mapato ya zaidi ya  shilingi bilioni 2.17  sawa na asilimia 124.91 katika kipindi cha mwaka 2023/2024.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Khalid Khalif  kwenye kikao cha Baraza la madiwani cha kujadili  taarifa ya Hesabu za mwisho  za Halmashauri kwa mwaka wa fedha za 2023/2024 kilichofanyika kwenye ukumbi  wa Ofisi ya Mkurugenzi Kilosa Mbambabay.

Amebainisha kuwa kati ya makusanyo hayo,mapato halisi ni shilingi bilioni 1.32 na mapato kutoka katika vyanzo zuiliwa ni zaidi ya shilingi milioni 859.

“Fedha za miradi ya maendeleo ambazo zimepokelewa katika kipindi hicho ni  11,857,058,019 ambazo zimetumika kwa ajili ya mfuko wa afya wa Pamoja,elimu bure, TASAF, SEUIP, P4R, UNICEF,CDCF,chanjo ya polio, umaliziaji wa maboma, shule shikizi,BOOST na swash’’,alisema.

Ameongeza kuwa mapato kutokana na kodi mbalimbali katika kipindi hicho yameongezeka kutoka shilingi 202,319,610 kwa mwaka 2022/2023 hadi kufikia shilingi 271,856,574 mwaka 2023/2024.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peres Magiri  akizungumza kwenye kikao hicho ameagiza kufanyika vikao vya kamati ya afya ngazi ya wilaya ambavyo vinazungumzia suala zima la afya kwa ujumla ikiwemo kutambua suala zima la virusi vya UKIMWI na vifo vya mama na mtoto.

 Mkuu wa Wilaya pia ameagiza ratiba ya vikao vya lishe ngazi ya Halmashauri  iandaliwe na  kuhakikisha vikao vinafanyika kwa wakati ili kutekeleza mikataba ya lishe katika ngazi zote hadi Kata ili kukabiliana na udumavu.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Stewart Nombo amewapongeza watumishi na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato hali iliyosababisha kuvuka malengo ya makusanyo kwa asilimia zaidi ya 124.

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa lina madiwani wa kuchaguliwa 20,viti ,maalum madiwani saba  na Mheshimiwa mbunge mmoja.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.