• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HALMASHAURI ya Songea yakamilisha ujenzi Kituo cha Afya Liganga

Imewekwa kuanzia tarehe: October 25th, 2022



WANANCHI wa vijiji vitatu vya kata ya  Liganga na  vijiji vingine vinavyopakana na kata hiyo katika Halmashauri ya wilaya Songea,wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya afya waliyokuwa wanakabiliana nayo kwa muda mrefu, kufuatia ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa katika kata hiyo kukamilika kwa asilimia 98.

Mkuu wa idara ya afya,ustawi wa jamii  na lishe wa Halmashauri hiyo Dkt  Geofrey Kihaule alisema,kituo hicho kinajengwa katika kijiji cha Selekano ambapo  kwa gharama ya Sh.milioni 500 ambazo zimetolewa  na Serikali kwa awamu mbili.

Dkt Kihaule alisema,katika awamu ya kwanza serikali ilitoa kiasi cha Sh.milioni 250 ambazo zilitumika kujenga jengo la wagonjwa wa nje(OPD)maabara,na kichomoea taka ambapo majengo hayo yamekamilika kwa asilimia  100.

Alisema,majengo hayo yanatarajiwa kufunguliwa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao  na  kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa magonjwa ya nje wanaofika kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za matibabu.

Kwa mujibu wa Dkt Kihaule,watumishi  watatu watakao fanya kazi katika kituo hicho wameshafika na kwa sasa wapo katika zahanati ndogo ya misheni ya Liganga wakisaidia kutoa huduma kwa wananchi huku wakisubiri kufunguliwa kwa kituo hicho.

Aidha alisema,katika awamu ya pili Halmashauri  imepokea  jumla ya Sh.milioni 250 kwa ajili ya kujenga majengo pacha ambayo ni ya huduma ya mama na mtoto,upasuaji pamoja na jengo la kufulia ambayo yote kwa sasa yamekamilika.

Dkt Kihaule,ameiomba serikali kuwasaidia kupata vifaa vikiwamo vya maabara  mapema ili waweze kuanza kutoa huduma, kwani majengo yote yamekamilika na  kinachosubiri ni kupata  vifaa vya upasuaji,maabara na vitanda kwa ajili ya kulaza wagonjwa.

Alisema,kituo hicho kinatarajiwa kuwahudumia watu wengi zaidi kuliko kituo chochote cha afya katika Halmshauri ya wilaya Songea wakiwamo wafanyakazi zaidi ya elfu nne wa shamba la kahawa la kampuni ya Aviv Ltd ambao wengi wanaishi katika kijiji cha Liganga.
Dkt Kihaule alitaja wanufaika wengine ni  wananchi wa kijiji cha Liganga,Seekano,wafungwa na askari wa gereza la Kitai,wafanyakazi wa migodi ya makaa ya mawe,wananchi wa kijiji cha Amanimakoro  kilichopo wilaya jirani  ya Mbinga, wananchi wa kijiji cha Mbinga Mhalule,Matomondo na Lipokela.

Alisema,kukamilika kwa kituo hicho ni ufumbuzi mkubwa sio kwa wananchi wa kata ya Liganga tu, bali hata kwa watu wengine wanaotumia barabara ya Songea-Mbinga ambao wakipata ajali na shida nyingine watakimbilia katika kituo hicho kwa ajili ya kupata msaada wa matibabu.
Mwenyekiti wa kijiji cha Selekano Magreth Haule,ameishukuru serikali kupitia Halmashauri hiyo kuwajengea kituo cha afya kwani awali walilazimika kutembea umbali mrefu na kutumia gharama kubwa Kwenda kupata matibabu maeneo ya mbali.

Amempongeza Mbunge wa JImbo la Peramiho na Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala  bora Jenista Mhagama,kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo  na kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Songea Neema Maghembe alisema,tayari wamepokea jumla ya watumishi 39  wa kada mbalimbali katika sekta ya afya ambao wamesharipoti na wanaendelea kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi.


Maghembe alisema,katika kipindi cha mwaka mmoja wamepokea Sh.bilioni 1 zinazotokana na tozo  kwa ajili ya kujenga vituo viwili vya afya katika kata ya  Liganga na Mgazini.

Aidha alieleza kuwa, wamepokea fedha nyingine  kiasi cha Sh.milioni 500 kwa ajili ya kujenga jengo la upasuaji na majengo mengine katika Hospitali ya Halmashauri iliyopo kijiji cha Mpitimbi ambayo imeshaanza kutoa huduma kwa wananchi wa Songea na wale wanaotoka nchi jirni ya Msumbiji.

Maghembe alisema, katika mkakati wa kusogeza huduma kwa wananchi wamefanikiwa kujenga zahanati katika kijiji cha Ndongosi kwa gharama ya Sh.milioni 50 na zahanati nyingine katika kijiji cha Makwaya kata ya Lilahi ambapo wananchi walilazimika Kwenda maeneo mengine kufuata matibabu.

Pia alisema, wamepokea kiasi Sh.milioni 104 ambazo zitatumika kuboresha mazingira ya kujifungulia kwa akina mama wajawazito katika zahanati  mbalimbali ambapo kwa sasa wananchi wa maeneo hayo wanaendelea kufurahia huduma bora za afya.

Maghembe amewaasa wananchi kutumia zahanati,vituo vya afya na Hospitali zinazojengwa kwenda kupata huduma bora za afya kwani serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili yao na  kuachana na mira  zilizopitwa na wakati zinazodai  ukiwa mtu wa kwanza kupata huduma kwenye vituo na Hospitali zinazojengwa  unaweza kupoteza maisha.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.