HALMASHAURI za Mkoa wa Ruvuma zimejipanga kuboresha sekta ya Michezo na kuepuka maandalizi ya zimamoto.
Akizungumza Afisa Michezo wa Mkoa wa Ruvuma Antony Luoga amesema katika hatua za uboreshaji wa Michezo itasaidia Mkoa kufanya vizuri katika Sekta ya Michezo kimkoa.
“Kila Halmashauri imeagizwa kuwa na vitalu ambavyo vitawaandaa wanamichezo kuepuka maandalizi ya zimamoto”.
Luoga amesema Shule ya Sekondari Mahanje iliyopo Halmashauri ya Madaba kuwa Shule ya Michezo na inapokea wanafunzi wenye vipaji vya michezo mbalimbali kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma ili kukuza vipaji vyao.
“Wanafunzi hawa ni wale waliofika ngazi ya Taifa na kufaulu mitihani yao ya Shule ya Msingi”.
Amesema juhudi za kuwashirikisha wananchi katika juhudi za kuchangia na kuendeleza Michezo katika Mkoa wa Ruvuma unaendelea pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki katika kufanya mazoezi na michezo mbalimbali ya asili ya Tanzania.
“Timu ya Majimaji kuwa katika mchakato wa kuwa kampuni ili kuboresha mwenendo wake”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 15,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.