KAMATI ya Siasa Mkoa wa Ruvuma imetembelea Shamba la Miti Wino katika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea lenye hekta 39,000.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho Mara baada ya kukagua Shamba hilo amebaini changamoto ya barabara kutopitika kwa urahisi wakati wa Mvua na amewaomba TARURA kuangalia uwezekano wa uboreshaji wa Barabara hiyo.
Mwisho amebaini pia changamoto ya uchomaji wa Moto katika maeneo ya Shamba hilo na ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa pale wanapotaka kuchoma mashamba yao ili TFS wawape mbinu ili Moto usisambae katika Mashamba hayo.
‘’Wananchi Muwe wastaarabu katika kuchoma Misitu Moto kwasababu TFS wanatoa Elimu halafu wananchi mnakuwa wakaidi mnapelekea kuharibu shamba la miti ambalo linategemewa kuingiza uchumi katika nchi yetu’’.
Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu Shamba la Miti Wino Grory Kasmir akisoma taarifa kwa kamati hiyo amesema hifadhi ya Msitu wa Wino iliendelezwa na TFS mwaka 2010 na kuhusishwa eneo dogo la msitu wa asili wenye ukubwa wa hekta 2,000 na mwaka 2014 hadi 2016 walipata maeneo vijiji vya Mkongotema na finga.
Kasmir amesema kuanza upandaji wa Miti hadi kufikia sasa jumla ya hekta 5,004.6 imepandwa miti ya jamii mbalimbali na sehemu kubwa ni miti ya misindano.
Mhifadhi ameeleza malengo makubwa ya kuanzishwa kwa hifadhi ya msitu wa Wino Pamoja na kuhifadhi mali asili zinazotaka kutoweka na vyanzo vya Maji Lupahila,Lutukila,Luhuhu Pamoja na Ziwa Nyasa.
Hata hivyo Kasmiri ameeleza faida ya Shamba hilo ikiwemo Ajira kwa watumishi wa kudumu 15 wamkataba 7 pamoja na vibarua 4,000 na Mazao ya Biashara kama Mbao,Nguzo za Umeme kwa siku za usoni ili kuongeza mapato ya Serikali Pamoja na kuboresha mazingira.
Mhifadhi ameeleza changamoto zinazojitokeza katika Shamba hilo ikiwemo matukio ya uchomaji wa Moto kwa kiasi kikubwa na kupunguza usimamizi endelevu wa shamba ,uandaaji wa Mashamba msimu wa Kilimo kwa kutumia Moto.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Novemba 12,2012.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.