• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HEKTA 40,000 kupandwa miti ya biashara Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: January 28th, 2021

MKOA wa Ruvuma umelenga kupanda miti ya biashara katika eneo lenye ukubwa wa hekta 40,000 hadi kufikia mwaka 2025.

Mshauri wa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe amesema  mradi huo unatekelezwa kwa miaka kumi kuanzia mwaka 2015,unatekelezwa kwa kupanda miti maeneo ya serikali kuu,serikali za mitaa,vyuo,shule na vijiji.

Challe ameitaja aina ya miti inayopandwa ni ile ambayo inafaa kwa ajili ya malighafi za viwanda vya mazao ya misitu ambayo ni misindano (pine),milingoti(Eucalyptus) na misaji(Teak).

‘Hadi kufikia mwaka 2020 jumla ya miti ya biashara iliyopandwa na wakala wa Huduma za misitu Tanzania(TFS) ni msitu wa hekta 4785,Halmashauri zilipanda miti hekta 425,vyuo na shule hekta 420 na watu binafsi hekta 23,964.

Amesema jumla ya mashamba yote ya miti yaliyopandwa katika kipindi hicho ni hekta 29,194 sawa na asilimia 56.1 ya lengo.

Kwa mujibu wa Mshauri huyo wa Maliasili na Utalii,Mkoa wa Ruvuma unalenga kuanzisha mashamba mapya mawili ya miti ya misaji katika Wilaya za Tunduru na Nyasa.

Kwa upande wake Mratibu wa kuendeleza Program ya mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu(FORVAC) Mkoa wa Ruvuma Marcel Mtunda  amesema  wameandaa miche ya miti ya biashara aina ya misaji,pine na Eucalyptus ipatayo 4,000,000 ambayo itapandwa maeneo maalum yaliyotengwa na Mkoa yakiwemo Ifinga, Liuli, Liumbe, Upolo,Mpepo,kipiki na Kihangamahuka.

Amesema Mkoa unatekeleza mradi wa kuongeza thamani mazao ya misitu na nyuki kwa kushirikiana na FORVAC  na kwamba mradi unatekelezwa katika wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma.

“Mradi huu utawezesha vijiji kutunza misitu ya hifadhi ya vijiji na kuwawezesha kupata faida kwenye misitu hiyo,hadi sasa wilaya ya Tunduru imeshapata mashine moja ya kuchana mbao ambayo imeanza kufanyakazi katika kijiji cha Sautimoja’’,alisema Mtunda.

Hata hivyo amesema Mkoa kwa kushirikiana na FORVAC imeomba mashine nyingine tatu ili zitumike katika wilaya za Namtumbo,Songea,Mbinga na Nyasa na kwamba mradi utasaidia kupunguza gharama za serikali kutekeleza miradi ya kimkakati ya kujenga shule,zahanati na madawati.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Januari 28,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.