• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HIFADHI ya Matogoro ina fursa lukuki za utalii

Imewekwa kuanzia tarehe: January 27th, 2025


Hifadhi ya Msitu Asili Matogoro yenye mandhari ya kuvutia ni kichocheo adhimu na muhimu cha kukuza utalii katika mikoa ya kusini hususan mkoa wa Ruvuma kutokana na  kubeba hazina kubwa ya kihistoria ikiwemo uwepo wa mapango makubwa yaliyotumika wakati wa vita ya majimaji.

Haya yamebainishwa na Naibu waziri wa maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) alipofanya ziara ya kujionea fursa za kiutalii zinazopatikana katika Hifadhi ya Msitu Asilia Matogoro iliyopo Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma.


Aidha, hifadhi hii ya Msitu Asilia na milima yake imebeba jukumu kubwa la uhai na ustawi wa watanzania kutokana na ukweli kuwa Hifadhi hii ni chanzo cha mito mitatu mikubwa na muhimu ambayo ni Ruvuma unaomwaga maji yake kwenye bahari ya Hindi, Luwegu ambao unachangia asilimia 19 ya maji kwenye mto Rufiji na kisha kuingia bahari ya Hindi, na Mto Luhira ambao ni chanzo cha mto Ruhuhu ambao unamwaga maji yake kwenye Ziwa Nyasa.


Mheshimiwa Kitandula alitoa wito kwa wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza katika eneo hilo lenye mandhari nzuri na ya kuvutia ambayo inafaa kwa utalii wa kupanda milima, utalii wa picha, utalii wa kuruka kwa puto na utalii wa ikolojia kukimbilia na kuikumbatia fursa hiyo.

Vilevile Mhe. Kitandula ameutaka uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambao unasimamia eneo hilo kulitangaza kwa kuliunganisha na matamasha mbalimbali ya vijana yanayofanyika katika mkoa wa Ruvuma kwa kuwashawishi washiriki watembelee Hifadhi ya Msitu Asilia Matogoro. Ninauhakika mandhari niliyoiona hapa maharusi wengi wangetamani kufika kileleni na kufanyia sherehe zao za harusi mahali hapa.

Vilevile , Mhe. Kitandula akihitimisha ziara yake, ameushukuru Uongozi wa Mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano unaoutoa kwa taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii hasa kwenye kukabiliana na changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.