• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

IDARA ya Uthibiti Ubora wa Shule ,Jicho la ubora wa elimu nchini

Imewekwa kuanzia tarehe: March 23rd, 2025

Na Albano Midelo

Katika jitihada za kuinua ubora wa elimu nchini Tanzania, Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kuhakikisha viwango vya elimu vinaimarika.

Idara hii, ambayo ipo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu bora.

Maono ya Rais na Jitihada za Idara

Afisa Mthibiti Ubora wa Shule wa Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma, Mwl. Rehema Haule, anasisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa mwanga mkubwa kwa sekta ya elimu na kwamba  Kupitia maono yake, Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule inatekeleza mikakati madhubuti ili kuboresha elimu katika ngazi zote.

“Idara hii ni jicho la Wizara ya Elimu kwani ina jukumu la kusimamia, kufuatilia, na kuboresha viwango vya elimu nchini’’,anasema na kuongeza kuwa Kupitia juhudi hizo, serikali imeweza kufanikisha malengo mengi ya elimu bora, ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Muundo wa Idara na Majukumu Yake

Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule inaongozwa na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule, akisaidiana na Wakurugenzi Wasaidizi katika vitengo vya Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari, Vyuo vya Ualimu, na Maendeleo ya Wananchi.

Kulingana na Haule,Katika ngazi ya Halmashauri, kuna Maafisa Uthibiti Ubora wa Shule wanaoshirikiana na wathibiti wengine ili kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Mwl.Haule anabainisha kuwa Katika utekelezaji wa majukumu yake, Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule inatekeleza kazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kufanya tathmini ya jumla ya shule kwa kutembelea na kujiridhisha kuhusu hali halisi ya shule na Kusimamia na kuinua viwango vya elimu katika shule za awali, msingi, sekondari, na vyuo vya ualimu.

Majukumu mengine anayataja kuwa ni Kufanya tathmini ya ufuatiliaji ili kuhakikisha maboresho yaliyopendekezwa yanatekelezwa,Kufanya tathmini maalumu kwa madhumuni mbalimbali kama usajili wa shule na kushughulikia changamoto zinazojitokeza na Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau wa elimu kila inapohitajika.

Kwa mujibu wa Afisa Uthibiti huyo,majukumu mengine ni Kuwajengea uwezo walimu katika kutekeleza majukumu yao, hususan mbinu bora za ufundishaji.Kuandaa ripoti za tathmini na kuzifikisha kwa wadau wa elimu kama vile Kamati za Shule, Maafisa Elimu wa Kata, na Wizara ya Elimu na Kufanya tafiti za kutatua changamoto katika sekta ya elimu.

Umuhimu wa Elimu Bora kwa Maendeleo ya Taifa

Maendeleo ya taifa lolote yanategemea kwa kiasi kikubwa ubora wa elimu inayotolewa kwa wananchi wake. Elimu bora inawapa watu ujuzi na maarifa, hivyo kuwa msingi wa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (toleo la 2023) inaeleza kwa kina umuhimu wa uthibiti wa ubora wa elimu, jambo linalosisitizwa na Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule.

Kwa mujibu wa Idara hiyo, wadau wote wa elimu wanapaswa kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha kuwa viwango vya elimu vinaendelea kuimarika.

Ofisa Uthibiti huyo wa Ubora wa shule katika Wilaya ya Nyasa anawahimiza wadau wote wa elimu kuwasiliana na ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule kabla ya kuanzisha shule au kufanya maamuzi muhimu kuhusu elimu ili kupata ushauri wa kitaalamu.

Hata hivyo anasema Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule inaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa elimu inakuwa chachu ya maendeleo ya taifa. Kupitia maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu, Ubora wa elimu nchini unaendelea kuimarika.

Haule anawakaribisha wadau wote wa elimu, wakiwemo walimu, wazazi na wananchi kwa ujumla, kutembelea ofisi zao ili kupata ushauri wa kitaalamu na kusaidia kuleta mageuzi chanya katika sekta ya elimu Tanzania

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.