Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, imepita pia katika Wilaya za Namtumbo na Tunduru mkoani Ruvuma.
Hifadhi hii ni miongoni mwa hifadhi kubwa zaidi za wanyamapori nchini Tanzania na barani Afrika.
Hifadhi hii ni sehemu ya iliyokuwa Selous Game Reserve, mojawapo ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyopo chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO.
Imepewa jina la Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 2019 ili kumuenzi kwa mchango wake katika uhifadhi wa maliasili na mazingira.
Hifadhi hii inajulikana kwa bioanuwai yake ya kuvutia, ikiwa na idadi kubwa ya wanyamapori kama tembo, simba, chui, mbwa mwitu wa Afrika, viboko, na mamba, pamoja na aina mbalimbali za ndege. Mito kama vile Rufiji inapita kwenye hifadhi hii, ikitoa mazingira mazuri kwa wanyama na viumbe wengine wa majini.
Hifadhi ya Nyerere pia ni maarufu kwa shughuli za utalii wa kiikolojia, kama vile safari za magari kwa ajili ya kuona wanyama, safari za mitumbwi kwenye mto Rufiji, na matembezi ya miguu kwa mwongozo wa watalamu wa uhifadhi.
Ni sehemu muhimu kwa uhifadhi wa maliasili na hutoa fursa kwa watalii na wapenzi wa mazingira kushuhudia mandhari za kipekee za Afrika pamoja na wanyama katika makazi yao asilia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.