Shirika la BRITEN limeratibu utoaji elimu ya kilimo kuhusu mbegu bora na mbolea kupitia shamba darasa la zao la mahindi kwa wakulima wa Mtaa wa Masigira Kata ya Tanga Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Elimu hiyo imetolewa ikiwa ni siku ya mkulima ambayo katika Manispaa ya Songea imefanyika katika kata ya Tanga ambapo kampuni mbalimbali za uzalishaji mbegu za mahindi zilitoa elimu ya ubora wa mbegu za mahindi na mbolea.
Afisa Mauzo na Bwana Shamba kutoka Kampuni ya Seedco Tanzania Limited Erick Ng,oro ameitaja mbegu ya mahindi ya chapa Tembo kuwa inafanya vizuri katika Mkoa wa Ruvuma ambayo inamwezesha mkulima kuzalisha mahindi kati ya gunia 50 hadi 55 kwa hekari moja hivyo ameshauri wakulima kuitumia mbegu hiyo kwa kuzingatia kanuni za kilimo ili kutoa matokeo makubwa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.