Jamii imeshuriwa kuchukua tahadhari na kuzingatia kanuni taratibu na sheria inayozuia kula mizoga au nyama isiyokaguliwa na wataalam wa mifugo ili kijikinga na magonjwa ya milipuko.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dr Erick Kahise wakati wa mahojiano ofisini kwake mjini Peramiho.
Dr Kahise ametaja mfano wa magonjwa ambayo yanatokana na kutozingatia kanuni za afya ni minyoo ya nguruwe ambayo hukaa ndani ya ubongo kwa muda mrefu na kusababisha kifafa.
Magonjwa mengine ni kutupa mimba kwa ng’ombe ambao binadamu anaweza kupata na dalili zake zinafanana na za malaria,kunywa maziwa mabichi ambayo yametokana na ng’ombe mwenye vimelea vya TB (micobacterium bovis).
Ametahadharisha kuacha kuishi na wanyama ndani ya nyumba moja na kuacha mifugo kuzurura hovyo kama mbwa ni hatari kwa afya ya binadamu kwa sababu nao husambaza magojwa kama kichaa cha mbwa ambacho kinaonekana kuwa tishio kwa uhai na hustawi wa binadamu.
“Ikitokea mnyama amekufa wananchi waache tabia kukimbilia kula nyama badala yake watoea taarifa kwa mamlaka husika ili taratibu za kitaalam ziweze kufanyika”,amesisitiza Dr Kahise.
Dr kahise ametaja mikakati ya kudhibiti magonjwa hayo kuwa ni pamoja na uchinjaji na uuzaji wa nyama kufanyika katika maeneo rasmi yaliyoruhusiwa na Serikali.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dr.Jofrey Kihaule amesema katika klpindi cha kuanzia mwaka 2019 hadi Oktoba 2020 jumla ya watu 340 waling’atwa na mbwa kati ya hao watu 20 walithibitika kuugua kichaa cha ,mbwa na wamepata matibabu.
Jacquelen Clavery
Afisa Habari, Songea DC.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.