SERIKALI imetoa kiasi cha Sh.milioni 630,340,507.00 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la huduma za dharura(EMD)kwa awamu mbili katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma(Homso).
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Magafu Majura amesema hayo , wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim.
Dkt Majura alieleza kuwa,katika awamu ya kwanza mkoa wa Ruvuma ulipokea kiasi cha Sh.milioni 250,910,500.00 na awamu ya pili imepokea Sh.milioni 379,430,007.
Kwa wa Dkt Majura ni kwamba,mradi huo umetekelezwa kwa njia ya force Akaunti ambapo gharama za ununuzi wa vifaa vya ujenzi ni Sh.milioni 557,527,942 na gharama za ufundi wa jengo hilo ni Sh.milioni 72,812,565.
Alisema,mradi ulianza kutekelezwa mwezi Julai 2020 kwa kuvunja baadhi ya majengo na kukamilika mwezi Septemba 2021,ambapo kazi zote zilizopangwa kutekelezwa zimekamilika kwa asilimia 100 na jengo limeanza kutumika.
Alisema,lengo la kujenga jengo hilo ni baada ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la wateja/wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali hiyo,hususani wenye magonjwa ya dharura na changamoto ya kutokuwa na jengo maalum kwa ajili ya huduma za wagonjwa wa dharura mbali ya kutumia eneo finyu la wagonjwa wa nje(OPD).
Alisema,hali hiyo ililazimu serikali ya mkoa wa Ruvuma kuanza mchakato wa kuiomba wizara ya afya kujengewa jengo lenye nafasi kubwa ya kuweza kuwahudumia wagonjwa hao wa dharura.
Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim,ameipongeza serikali ya mkoa wa Ruvuma na wasimamizi wa mradi huo kwa kazi nzuri kwani umejengwa kwa viwango na ubora unaotakiwa na unalingana na fedha zilizotolewa.
Alisema,mradi huo ni wa mfano katika mkoa wa Ruvuma na kuwataka wananchi na watumiaji wengine(watumishi)wa Hospitali ya Rufaa kuhakikisha wanatunza jengo hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.