Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt Emanuel Nchimbi ameagiza sekta ya michezo kuendelezwa kwa kuwa watanzania wengi wakiwemo wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wanapenda michezo.
Dkt. Nchimbi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ziara yake mjini Songea.
Dkt Nchimbi amesikitishwa namna ambavyo viongozi wa Michezo Mkoa wa Ruvuma walivyo kwamisha Maendeleo ya michezo.
Hata hivyo Balozi Dkt. Nchimbi amebainisha baadhi ya mifano ambayo yeye alipokuwa Mbunge wa jimbo la Songea mjini alishuhudia ikiwemo viongozi wa Timu ya Mkoa wa Ruvuma ya Majimaji FC kuhujumiwa na baadhi ya viongozi wa wakati huo wa Timu ya Majimaji Fc
Katibu Mkuu huyo amewataka Watanzania kwa ujumla kuacha tabia za ubadhirifu na wizi hasa katika michezo ili kuendelea kuboresha michezo nchini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.