Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi amezuru kaburi la mmoja wa waasisi wa chama cha TANU (Ambacho kiliungana na chama cha ASP mwaka 1977 na kuanzishwa CCM) Costantine Osward Millinga (LIKAPU) aliyefariki Machi 5, 2018 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.
Mbali ya kuzuru kaburi hilo na kuweka shada la maua, Dkt. Nchimbi alifika nyumbani kwa marehemu na kutoa pole kwa mjane Maria Costantine Millinga na kusaini kitabu cha kumbukumbu akiwa hapo.
Akiwa hapo, Dkt. Nchimbi ameahidi CCM kuendelea kuenzi mema yaliyofanywa na waasisi wa TANU pamoja na kuwaenzi wote waliosaidia kwenye kuanzishwa kwake na kubeba dhamana ya kupigania uhuru wa Tanganyika ambao ulichangia kupatikana kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964.
Enzi za uhai wake, marehemu Likapu aliyefariki akiwa na umri wa miaka 93 alikuwa mmoja wa washauri wa chama hicho.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.