Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Profesa Riziki Shemdoe amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa wanawaruhusu na kuwawezesha Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri kushiriki kikao cha Maafisa Habari kilichopangwa kufanyika jijini Mbeya wiki ijayo.
Agizo hilo limetolewa leo na Katibu Mkuu wakati wa kuhitimisha Mkutano wa 11 wa Umoja wa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) uliofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.Katibu Mkuu amewataka Viongozi hao kuwaruhusu Maafisa Habari na kuwawezesha nyenzo mbalimbali ili washiriki kikamilifu kwenye mkutano wa Maafisa Habari uliopangwa kufanyika kuanzia tarehe 24 hadi 28 Mei 2021 jijini Mbeya
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.