Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Khamis Hamza Khamis ameagiza hatua kali za kisheria kuchukuliwa kwa wote wanaomwaga madini ya makaa ya mawe barabarani na kuchafua vyanzo vya maji na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi.
Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo wakati anazungumza kwenye majumuisho ya Timu ya mawaziri wanane wa kisekta kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Awali Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Odo Mwisho alielezea uchafuzi wa mazingira unaotokana na madini ya makaa ya mawe ambapo baadhi ya madereva wamekuwa wanamwaga makaa ya mawe barabarani na kuleta athari za kimazingira.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.