Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha TARI kilichojengwa mwaka 1959 katika eneo la Ndengu, Wilayani Mbinga kwenye Mkoa wa Ruvuma kimeelekezwa kufufuliwa ili kianze shughuli za uzalishaji wa mbegu za ngano, tafiti za mbegu za mpunga na muhogo, pamoja na upimaji wa afya ya udongo.
Ameelekeza hayo Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo aliposimama kukikagua wakati wa ziara yake katika Wilaya za Nyasa na Mbinga mkoani Ruvuma
Waziri Bashe ameongeza zaidi kuwa Mkurugenzi wa TARI Uyole, Dkt. Tippe ahakikishe Kituo hicho kitakufufuliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na Wakala wa Mbegu Bora za Kilimo (ASA) ili kuzalisha mbegu kwa wingi kusaidia wakulima wa Wilaya hizo mbili ambao wanafanya kilimo cha kahawa, mpunga, muhogo, michikichi, mahindi na mazao mengine.
Naye Dkt. Tippe ameomba Watumishi wa tatu wa Kituo hicho wapatiwe pikipiki kusaidia usafiri; ambapo ombi hilo Mhe. Waziri Bashe aliridhia na kuielekeza Wizara ya Kilimo iwapatie pikipiki tatu.
Aidha, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) nayo imeelekezwa kusaidia upatikanaji wa mbolea za ruzuku ili wakulima wa eneo hilo waweze kunufaika
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.