• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UKARABATI na upanuzi kiwanja cha Ndege Songea wafikia asilimia 97

Imewekwa kuanzia tarehe: January 10th, 2023

KAZI ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha Ndege Songea mkoani Ruvuma imefikia asilimia 97 na kiwanja hicho kinatarajia kukabidhiwa serikalini Januari 30 mwaka huu.

Akitoa taarifa ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho kwa Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma,Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi  amesema serikali ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 37 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

Amesema mradi huo ulitekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya CHICCO toka nchini China kwa miezi 20 kuanzia Septemba 2019 hivyo unatarajiwa kukabidhiwa mwezi huu na ndege zinatarajiwa kuanza kutua usiku 

Amezitaja kazi ambazo zimefanyika kuwa ni ukarabati na utanuzi wa njia ya kurukia ndege kutoka urefu wa meta 1625 na upana wa meta 30 hadi kufikia urefu wa meta 1740 na upana wa meta 30.

“Kazi nyingine zilizofanywa ni upanuzi wa maeneo ya usalama wa ndege,ukarabati na upanuzi wa eneo la maegesho ya ndege,ujenzi wa eneo jipya  la maegesho ya ndege kwa dharura,jengo jipya la abiria na upakaji wa rangi wa alama za kiwanja’’,alisema Mhandisi Mlavi.

Amezitaja kazi nyingine kuwa ni ujenzi wa mitaro,ujenzi wa  uzio wa kuzunguka kiwanja,ujenzi wa barabara ya ndani ya kukagua usalama wa kiwanja,ufungaji wa taa za kuongozea ndege,ufungaji wa vifaa vya mawasiliano ya anga na ujenzi wa jengo la mitambo ya umeme.

Meneja huyo wa TANROADS Mkoa amezitaja kazi zilizoongezeka kuwa ni utanuzi wa njia ya kurukia ndege,ujenzi wa barabara ya nje ya kukagua usalama wa kiwanja,ujenzi wa jengo la muda la mitambo ya mawasiliano na anga na uongozi wa ndege.

Hata hivyo amesema utekelezaji wa mradi kwa ujumla umefikia asilimia 97 na kwamba kazi zilizosalia ni mitambo ya umeme,mitambo ya kusukuma maji ,taa za kuongozea ndege na vifaa vya usambazaji mawasiliano ya anga ambapo amesema kazi zote zinatarajia kukamilika Januari 30,2023.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemshukuru Rais kwa kutoa fedha za ukarabati wa kiwanja cha ndege na miradi mingine mikubwa ya kimkakati kukamilika mkoani Ruvuma.

Kanali Thomas amesema wananchi sasa wanahitaji kuona miradi yote inakamilika kwa asilimia  100 na kwamba wananchi wa Ruvuma wanatamani kuona sasa ndege zinatua usiku katika kiwanja cha Songea.

Ameyataja mahitaji ya abiria wanaotumia ndege katika Mkoa wa Ruvuma ni makubwa ambapo hivi sasa wanahitaji safari za usiku na mchana kwa kutumia ndege za ATCL.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amesema Mkoa wa Ruvuma umepata uwanja wa kisasa wa ndege ambao utawezesha wasafiri  kufika Songea mchana na usiku  na kufanya biashara na kurejea Dar es salaam.

Amesema Mkoa wa Ruvuma una vivutio vya utalii na uwekezaji ambavyo sasa unaweza kuvifikia kwa haraka kwa kutumia usafiri wa anga.

Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege Songea Jordan Mchami amesema kabla serikali kuleta ndege za ATCL,wananchi wenye uwezo walisafiri kwa gharama kubwa Kwenda na kurudi  Songea hadi Dar es salaam ilikuwa ni shilingi milioni moja.

Amesema  hivi sasa kupitia ndege wa ATCL Kwenda na kurudi Songea hadi Dar es salaam ni kati ya shilingi laki tatu hadi nne kwa safari ya  Kwenda na kurudi.

Amesema kiwanja cha Songea kina uwezo wa kutua ndege aina ya Bombadier yenye uwezo wa kubeba abiria 76 ambayo mara nyingi imekuwa inakuja na abiria 76 kwenda na abiria 76.

“Ndege inajaa hivyo tunatoa rai kwa kampuni nyingine za ndege kuanzisha safari na ATCL kuongeza safari za ndege ikiwezekana hata kila siku, tunatarajia kuanza safari za usiku taa zimeshafungwa tunasubiri kufanya majaribio ya kutua usiku ili hatimaye ndege zianze kutua usiku’’,alisema Mchami.

Uwanja wa ndege wa Songea ni miongoni mwa viwanja  bora vya ndege Tanzania ambao ulijengwa kati ya mwaka 1974 hadi 1980.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Januari 10,2023

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.