MKOA wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambayo imebarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa na vivutio vya aina zote za utalii,ambazo ni utalii wa ikolojia na utamaduni.
Mkoa wa Ruvuma una mapori manne ya wanyamapori ambayo ni sehemu ya mfumo wa Selous.Mapori hayo ni Selous ambalo hivi sasa ni Hifadhi ya Taifa ya Nyerere lenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000,Pori la Liparamba lenye kilometa za mraba 571,Gesimasoa lenye kilometa za mraba 764 na Litumbandyosi lenye kilometa za mraba 464.
Hata hivyo utafiti umebaini bado kuna vivutio vingi ambavyo havijaibuliwa na kutambuliwa ili kutoa fursa za uwekezaji kwa watalii toka ndani na nje ya nchi.
Afisa Maliasili wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema vivutio hivyo vikiendelezwa vinaweza kuchangia pato la Taifa na kuinua uchumi wa wananchi na kwamba kinachotakiwa ni kuboresha miundombinu ya barabara na hoteli za kitalii ili kuvutia watalii kuvifikia vivutio hivyo.
Hatua mbalimbali zinachukuliwa na serikali kuanzia serikali ya awamu ya Tano na sita kuhakikisha miundombinu mbalimbali inaboreshwa katika Mkoa wa Ruvuma ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, ambapo hivi sasa wawekezaji wameanza kuonesha nia ya kuwekeza katika Mkoa wa Ruvuma na kwamba Mkoa umeunganishwa kwa barabara za lami katika wilaya zake zote,pia usafiri wa anga na majini umeboreshwa
Pia serikali imetoa mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Ruvuma ambao ulizinduliwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa mwaka 2019. Mwongozo huo unapatikana kwenye tovuti ya Mkoa wa Ruvuma ambayo ni www.ruvuma.go.tz
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.