Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 513 kwa ajili ya kujenga shule mpya ya msingi Ligoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
Taarifa ya ujenzi wa shule mpya ya msingi Ligoma inaonesha kuwa ujenzi huo unaendeshwa na fedha kutoka selikari kuu kwa kupitia mradi wa BOOST ambapo umelengo kujenga vyumba vya madarasa 16, jengo la utawala, matundu ya vyoo ishirini na nne pamoja na kichomea taka.
“wananchi wameshiriki kwa hatua mbalimbali kama vile usafishaji wa eneo la utekelezaji, uchimbaji wa msingi, usombaji wa tofari na maji pamoja na kusomba mchanga tripu 80 wenye thamani ya fedha zaidi shilingi milioni 6”, imeeleza taarifa hiyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa hiyo mradi umefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake na upo katika hatua mbalimbali za umaliziaji Pamoja na utengenezaji wa samani kama madawati, viti, meza, uwekaji wa bembea kwa madarasa ya Awali pamoja na kukamilisha ujenzi wa kichomea taka.
Ni ukweli usiopingika kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya maendeleo makubwa katika kijiji cha Ligoma kwa kuwajengea shule mpya ya msingi ambayo itasaidia jamii hiyo kupata elimu bora kwenye mazingira salama na rafiki kwa maendeleo endelevu.
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.