Umoja wa Wanawake kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma lMachi 6, 2023 wametembelea na kutoa zawadi kwa wanafunzi 69 wenye mahitaji maalum katika Shule ya msingi ya Ruhila iliyopo kata ya Mshangano Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
Akikabidhi zawadi hizo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye ni Afisa Tawala kutoka Boma kuu, Amina Tindwa, ambapo amesema wameguswa kuja kuwatembelea na kutoa zawadi hizo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani
kimkoa maadhimisho hayo yatafanyika wilayani Nyasa Machi 8,2023 kwenye viwanja vya Bandari ambapo mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ubunifu na Mabadiliko ya Kiteknolojia Chachu katika Kuleta Usawa wa Kijinsia”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.