Maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamepewa mafunzo kuhusu usimamizi na utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana, na wenye ulemavu.
mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Kilimo mjini Namtumbo yamehusisha maafisa maendeleo ya jamii kutoka kata zote 21 za Wilaya ya Namtumbo.
Mafunzo yamelenga kuimarisha uelewa kuhusu mikakati ya usimamizi wa maendeleo ya jamii, hususani katika kusimamia mikopo ya asilimia kumi kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Namtumbo Juma Njelu amesisitiza umuhimu wa mikopo hiyo katika kuboresha maisha ya wanajamii, huku akiwataka maafisa hao kuzingatia mafunzo hayo ili kuboresha zaidi Utendaji kazi wao katika kusimamia mikopo hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.