Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile amewataka Maafisa Ugani wa kilimo Wilaya ya Songea wahakikishe wanatekeleza wajibu wao katika kusimamia wakulima na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora.
Ndile amesema hayo wakati wa ugawaji wa vitendea kazi kwa wataalamu wa Ugani wa kilimo Wilaya ya Songea iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kuboresha utendaji kazi katika sekta ya Kilimo.
Amesisitiza kuwa wajibu wa kila afisa kilimo kuhakikisha anasimamia shughuli za kilimo na kutoa ushauri kwa wakulima namna ya kulima kilimo chenye tija pamoja na kutambua aina ya udongo katika shamba lake, aina ya mazao yanayostahili kulimwa katika shamba lake, kupanda kwa wakati, kupalilia kwa wakati, pamoja na kuweka mbolea kwa wakati.”
Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa kwa wataalamu hao ni pamoja na, Kwa Manispaa ya Songea wamepkea Ganboot pair 28, Rain Coat 28, Pump Sprayer 28, Madaba wamepokea Soil Scanner 1, Printer 1, Desktop 1, Ganboot pair 17, Rain Coat 17, Pump Sprayer 17, Kishikwambi 1, pamoja na Lamination Machine 1, Kwa Halmashauri ya Wilaya wamepokea, Soil Scanner 1, Printer 1, Desktop 1, Ganboot pair 39, Rain Coat 39, Pump Sprayer 39, Kishikwambi 1 Lamination machine 1.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile akizungumza baada ya kugawa vifaa kwa maafisa ugani Manispaa ya Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.