Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mary Makondo amewaasa maafisa Ugani wa Serikali kuwajibika na kuwawezesha wakulima ili kuongeza uzalishaji wa zao la Soya katika Mkoa wa Ruvuma.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha kujadili uzalishaji wa zao la soya kilichofanyika katika ukumbi wa Cottage heritage Mjini Songea.
"Bado tunajitihada kubwa za kufanya na tuwajibike zaidi, ubunifu zaidi, tufanye utafiti zaidi, tusiridhike na pale ambapo tumefikia, wale watumishi wa Serikali tufanyeni wajibu wetu wa kuwawezesha wakulimai" ,alisema.
Katibu Tawala amewasisitiza maafisa Ugani i kujenga mazingira wezeshi kwa wakulima, kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Sanjari na hayo ameziomba Taasisi za fedha kuendelea kutoa elimu na kuwa tayari kuwawezesha wakulima katika uzalishaji wa zao la Soya.
Zao la soya hutumika kutengeneza vyakula vya binadamu, mifugo, matumizi katika viwanda vya dawa na matumizi mengineyo..
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.