Maafisa ushirika wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wametakiwa kutokuwa chanzo cha kuanzisha migogoro katika vyama vya ushirika ambavyo vipo katika wilaya hiyo ambapo sasa kumekuwa na migogoro inayopandikizwa katika vyama hivyo hasa unapo karibia muda wa uchaguzi wa viongozi wa vyama vya ushirika.
Akitoa maagizo hayo kwenye mkutano mkuu wa 21 wa mwaka wa chama kikuu cha ushirika cha Mbinga (MBIFACU) ambacho kinasimamia zao la kahawa mkuu wa wilaya ya Mbinga Bi Aziza Mangosongo amesema migogoro ambayo ipo kwenye vyama vya ushirika vya wilaya ya Mbinga kwa sehemu kubwa inaletwa na maafisa ushirika wa wilaya hiyo hivyo amewataka maafisa hao wawe sehemu ya kutatua migogoro na sio sehemu ya kuchochea migogoro.
Moja ya sababu ya vyama vya ushirika kuwa na migogoro ni malipo ya fedha ambapo baadhi ya wakulima wa kahawa wa wilaya ya Mbinga wamekuwa wakipeleka malalamiko kwenye chama kikuu cha ushirika cha Mbinga ambapo kaimu meneja wa chama kikuu cha ushirika Mbinga (MBIFACU) bwana Faraja Komba amesema chama hicho kimekuwa kikishughulikia changamoto hiyo ya malipo
Kutokana na kuwepo na changamoto ya migogoro ambayo ipo kwenye vyama vya ushirika wilaya ya Mbinga baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ushirika Mbinga (MBIFACU)wamewaomba viongozi kutoa elimu kwa wakulima ili migogoro hiyo iweze kuisha katika vyama hivyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.