Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mhandisi David Mkondya amepokea bomba za mradi wa Maji Mchomoro ambao kukamilika kwake kutawanufaisha wananchi wasiopungua 10000 wa vijiji vya Songambele na Mchomoro.
Kuwasili kwa vifaa hivyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa wilayani Namtumbo alimwagiza Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso kumfuatilia Mkandarasi Azhar anayetekeleza ujenzi wa mradi kwa sababu ya kusuasua kwa ujenzi wa mradi huo.
Waziri wa Maji alifanya kikao na Mkandarasi wa Mradi, viongozi wa wilaya, kata na wananchi na kumuagiza Mkandarasi kufanya kazi na kutekeleza mradi huo ndani ya miezi miwili, ambapo tayari vifaa vyote vinavyohitajika kwenye mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 vimepatikana.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.