• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MADABA waishukuru serikali kuwapatia maji safi na salama

Imewekwa kuanzia tarehe: October 30th, 2021

WANANCHI wa kijiji cha Igawisenga Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma,wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuanza kutekeleza mradi mkubwa wa maji unaokwenda kumaliza kero ya maji safi na salama katika kijiji hicho.

Akiongea kwa niaba  ya wananchi mbele ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Paul Ndikweje alisema, kwa muda mrefu  hawajawahi kupata maji ya bomba na hivyo kulazimika kutumia maji ya visima vya asili.

Alisema,kujengwa kwa mradi huo ni  faraja kubwa kwao  na unakwenda kuleta matumaini mapya kwa sababu walishakata tamaa  kupata maji ya bomba hasa ikizingatiwa umbali wa kijiji hicho kutoka makao  makuu ya wilaya na mkoa.

Aidha,ameomba Wakala wa maji vijijini Ruwasa wilaya ya Songea  kuwaunganishia maji kwenye nyumba zao kwani kufanya hivyo itakuwa rahisi kuchangia gharama na kuepusha migogoro, badala ya kujenga vituo vingi vya kuchotea maji(DP).

Alisema, wako tayari kulipia gharama za kuunganishiwa maji kwenye nyumba ambapo baadhi ya wananchi wameshajiandaa kuweka fedha kidogo kidogo na wanachosubiri ni kukamilika kwa mradi huo ambao wanaamini utaharakisha maendeleo.

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Songea Mathias Charles  alisema, mradi wa maji Igawisenga unatekelezwa kwa kutumia fedha za program ya malipo kwa matokeo na umesanifiwa kuhudumia wananchi 2,275 ifikapo mwaka 2041 ambao kwa sasa wanakadiriwa kuwa 1,336.

Alisema, gharama za  utekelezaji wa mradi huo ni Sh.216,831,229.00 ambao unatekelezwa na Ruwasa kwa kutumia wataalam wa ndani na ulianza Mwezi Februari 2021 na umefikia asilimia 80.

Kwa  pande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ameipongeza Ruwasa kwa kutekeleza mradi huo wa maji ambao utakapo kamilika utamaliza kero ya muda mrefu ya maji  safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Igawisenga.

Brigedia Jenerali Ibuge, ameagiza mradi huo ukamilike kama ulivyopangwa na kuitaka Ruwasa kushirikiana na Serikali ya kijiji na wananchi namna ya kuendesha mradi huo na kutunza vyanzo  kwani hatua hiyo itasaidia wananchi kuona mradi huo ni wao na kuulinda.

Alisema, maji ni muhimu sana kwa maisha ya Binadamu na maendeleo ya Nchi yetu,hata hivyo  hajaridhishwa kuona baadhi ya vyanzo vya maji havijalindwa kikamilifu na hivyo kuleta mashaka makubwa.

Alisema, Rais Samiha Suluhu Hassan amekusudia kwa dhati kumtua ndoo mama kichwani, ndiyo maana anaendelea kutoa fedha za kujenga miradi ya maji, hata hivyo  ni lazima wananchi  waelimishwe kuhusu madhara ya kulima na kufanya shughuli mbalimbali kwenye vyanzo na hifadhi za maji.

Brigedia Jenerali Ibuge ameitaka Ruwasa na uongozi wa Bonde la Ziwa nyasa ,kuhakikisha wanatumia rasilimali na nguvu kubwa kulinda vyanzo ili visiendelee kuvamiwa na wananchi na kuweka alama ambayo itazuia wananchi kuingia katika  maeneo hayo.

Ameigiza Halmashauri ya wilaya Madaba kupitia Baraza la Madiwani, kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji kwa faida ya sasa na baadaye.

.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.