MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Sajidu Idrisa Mohamed amewapongeza wananchi wa Kata ya Gumbiro kwa kuunga mkono jitihada za Rais Samia kwa usimamizi wa utekelezaji wa Miradi iliyoletwa katika Kata hiyo.
Ameyasema hayo wakati anasikiliza kero za wananchi wa Kijiji cha Ngadinda na kubainisha miradi iliyotekelezwa ikiwemo Madarasa mawili na matundu 3 ya vyoo kupitia mradi wa Boost jumla ya shilingi Milioni 53,100,000/=zimetumika, Shule ya Msingi Sokoine zaidi ya shilingi Milioni 34 zimetumika kwaajili ya ujenzi wa matundu 13 ya vyoo kupitia mradi wa SWASH.
“Mwaka 2023/2024 katika Kata hiyo wanatarajia kupokea zaidi ya shilingi Milioni 106 na kwaajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo”.
Hata hivyo Mkurugenzi ametoa rai kwa wazazi kuwalinda watoto na kuwahimiza kusoma ikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa fedha kwaajili ya kuboresha Miundombinu ya Shule.
Diwani Kata ya Gumbiro Gustaph Tindwa ameipongeza Serikali kwa kuleta fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata hiyo amesema mradi wa barabara utakaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 200 unaotekelezwa na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA).
“Hizo zote ni pongezi za Rais Samia,Mbunge wa Jimbo la Madaba na wewe Mkurugenzi wa Halmashauri ikiwa wananchi wa Kata ya Gumbiro wananufaika na miradi hiyo”.
Tindwa amesema pia mradi wa Maji unatekelezwa katika Kata hiyo kwa zaidi ya Shilingi Bilioni moja utakaowasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.