Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma Sajidu Idrisa Mohamed amewapongeza watumishi wa Halmashauri hiyo kwa utekelezaji kikamlifu afua za lishe hali iliyosababisha Hlmashauri hiyo kwa miaka miwili kufanya vizuri kitaifa.
Akizungumza kwenye kikao cha lishe katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mjini Madaba,Sajidu amesema katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2023/2024 mwaka 20221/2022 Halmashauri ya Madaba ilikuwa nafasi ya pili Kitaifa na mwaka 2022/2023 ilikuwa nafasi ya nne Kitaifa.
“Nawashukuru watumishi wenzangu kwa kufanya vizuri na kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri zaidi kimkoa na kitaifa”,alisistiza Sajidu.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Madaba Jovery Ntelagi,akitoa taarifa katika kikao hicho amesema Halmashauri inaendelea kupambana na lishe duni pamoja na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano ili kupunguza changamoto ya udumavu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.