katika picha ni MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dr.Julius Mwaiselage, akiwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Joel Mbewa, baada ya mazungumzo maalum kuhusu ujio wa madaktari bingwa hao wa saratani waliobobea katika fani hiyo mkoani Ruvuma.
Madaktari Bingwa hao wapo mkoani Ruvuma kwa ajili ya kuweka kambi ya siku saba katika Hospitali ya Rufaa ya Mt. Joseph Peramiho, kupitia mpango wa huduma za mkoba wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Huduma hiyo inalenga kufanya uchunguzi wa awali na kutoa matibabu kwa wananchi watakaobainika kuwa na saratani, ikiwa ni juhudi za serikali katika kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo hatari.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.