• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAHAKAMA Kuu kuhamia Dodoma

Imewekwa kuanzia tarehe: January 7th, 2023

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani amesema kuwa katika miezi mitatu ijayo kuanzia sasa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania yaliyopo Dodoma yatakuwa tayari yamekamilika kwa ajili ya watumishi wote kuhamia kwenye majengo yake mapya.

Alizungumza hayo leo katika halfa ya uzinduzi wa Mahakama za Wilaya ya Namtumbo, Ngara, Nanyumbu na  Tandahimba ilifanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Mhe. Siyani alisema hatua kubwa imepigwa katika ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania Dodoma ambapo ujenzi umefikia asilimia 78.

Aidha Mhe. Siyani alisema uzinduzi wa Mahakama za Namtumbo, Nanyumbu, Tandahimba na Ngara ni matokeo ya uwezeshwaji unaoendelea kufanywa na Serikali pamoja na usimamizi na utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano wa Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu wa Mahakama ya Tanzania.

Aliishukuru Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka misingi mizuri inayoiwezesha Mahakama kujenga miundombinu yake na hivyo kuwa na mazingira mazuri yanayoiwezesha Mahakama kutimiza wajibu wake.

Mhe. Siyani aliwahikikishia wananchi kwamba Mahakama itaendelea kujenga na kuboresha miundombinu yake katika ngazi zote.

Alisema ujenzi wa majengo hayo na mengine yanayoendelea kujengwa kote nchini, unaenda sambamba na uwekaji wa miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Mahakama.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel alisema tayari timu ya kwanza imeshahamia Dodoma tangu tarehe 29 Desemba 2022 na timu zinatarajiwa kuendelea kuhamia Makao Makuu ya Mahakama hivi karibuni.

Kwa upande wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha alisema ujenzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya ya Namtumbo, Nanyumbu, Ngara na Tandahimba umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.9 , fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani ya nchi

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.