• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAJENGO ya Huduma za Dharura EMD kufikia 116

Imewekwa kuanzia tarehe: April 9th, 2025

Serikali ya Tanzania imendelea kuboresha huduma za afya kwa kuongeza idadi ya hospitali zenye majengo ya kutolea huduma za dharura (EMD) kutoka 7 hadi kufikia 116 ndani ya miaka minne ikiwa ni ongezeko la hospitali 109.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo  wakati akifunga maadhimisho ya juma la afya kitaifa pamoja na kuzindua mfuko maalum wa ufadhili wa masomo kwa Madaktari Bingwa na Bobezi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Waziri Mhagama amesema kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya kutolea huduma za dharura kunapunguza vifo na kuokoa maisha kwa wagonjwa wa dharura na wa ajali.

Kuhusu huduma ya magari ya wagonjwa Waziri Mhagama amesema  idadi ya magari ya imeongezeka kutoka 540 mwaka 2020 hadi 1,267 jambo linalorahisisha huduma za dharurana kuwafikia wananchi wenye changamoto za afya.

“Magari haya yanakwenda kusaidia kusafirisha watu wenye changamoto za afya wakiwemo akinamama wenye changamoto za uzazi kwa haraka na kuwafikisha katika huduma za rufaa na hivyo kupunguza adha kwa wananchi na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika,” amesema Mhe. Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amezishukuru Sekta binafsi nchini kwa kuunga mkono Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi kuanzia ngazi ya msingi hadi ya Kitaifa.

“Kazi hii mnayoifanya kwa kushirikiana na serikali inatupeleka mahali pazuri kwa kuimarisha huduma za kinga kwa magonjwa, matumizi ya teknolojia zitakazotupelekea kutoa huduma stahiki kwa jamii,” amesema.

Naye Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema wanaposheherekea Siku ya Afya Duniani huku Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amepokea tuzo ya Global Gates Keepers Award inaonyesha taswira ya maendeleo makubwa katika sekta ya Afya akiwa ni miongoni mwa marais saba waliopokea tuzo hiyo ambapo ameielekeza kwa watumishi wa afya ikiwa ni kuthamini mchango wao katika kutoa huduma.

Akitoa salam za Ofisi ya Rais - TAMISEMI Naibu Waziri anayeshughulikia Afya , Dkt. Festo Dugange amesema Sekta ya Afya imeendele kuboresha mshikamano wa sekta hiyo ili kuhakikisha mwananchi wanaowahudumiwa  na wanapata huduma bora za afya popote alipo nchini.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.