MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa waumini na watanzania kwa ujumla kutoa kipaumbele katika kulinda mazingira kwa kupanda miti ya kutosha.
Makamu wa Rais ametoa wito huo mara baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Kiliani Jimbo Kuu Katoliki mjini Mbinga mkoani Ruvuma .
Amesema mkoa huo umeanza kuharibu mazingira kutokana na kuingizwa ng’ombe kupita kiasi pamoja na kukatwa miti ndani ya misitu iliopo mkoani humo.
Pia Makamu wa Rais amewasisitiza wazazi na walezi kuweka mkazo katika kuhakikisha watoto wanapata elimu ili kuwa na taifa lililoelimika na hivyo kuharakisha maendeleo.
Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbinga Mhashamu Baba Askofu John Ndimbo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na chama.
Makamu wa Rais yupo mkoani Ruvuma kwaajili ya ziara ya kikazi ya siku tano kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.