• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MALORI 1000 ya makaa ya mawe yanapita Songea kwa siku

Imewekwa kuanzia tarehe: July 28th, 2023

Serikali kujenga barabara ya mchepuko 
SERIKALI inatarajia kuanza kujenga barabara ya mchepuko kilometa 16 katika mji wa Songea ili kukabiliana na kero ya malori 1000 ya makaa ya mawe yanayopita mjini Songea kwa siku.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya  wakati anajibu ombi la wananchi wa Kata ya Lilambo Manispaa ya Songea la kuomba kujengewa barabara itakayopita nje ya mji ili kuepuka kero ya malori ya makaa ya mawe.

Naibu Waziri huyo amekiri kuwa barabara ya Songea hadi Makambako hivi sasa inabeba mizigo mingi na mizito hivyo serikali mwaka huu imeamua kuifanyia matengenezo makubwa kwa kuijenga upya ili iwe barabara ya kisasa.

“Mwaka huu tutaanza kujenga barabara ya lami kuanzia  Lutukira sehemu ambayo imechoka sana hadi Songea mjini,ikiwa ni Pamoja na  kujenga barabara ya mchapuko Songea mjini yenye urefu wa kilometa 16’’,alisema Naibu Waziri.

Amesema barabara hiyo ya mchepuko itasaidia magari makubwa kupita nje ya nchi badala ya kupita katikati ya mji na kwamba barabara za  mchepuko zitapita sehemu tatu ambazo amezitaja kuwa ni eneo la Namanditi,Msamala na Sogea .

Amesema serikali imefanya tathmini ya fidia kwa wananchi wote waliopitiwa na barabara ya mchepuko ambapo tayari serikali imeandaa fedha za kuwalipa fidia zaidi ya shilingi bilioni nne ambazo zipo tayari hazina.

Hata hivyo amesema wakati ujenzi wa kipande hicho unaendelea serikali itaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa kipande cha barabara ya kutoka Lutukira hadi Makambako.

Amesema licha ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 37 za upanuzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Songea,mwezi Septemba mwaka huu serikali italeta gari la kisasa za Zimamoto kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Songea.

Mbunge wa Songea mjini na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Damas Ndumbaro  kwa niaba ya wananchi wa Songea  ameishukuru serikali kwa  kutenga bajeti katika mwaka huu wa fedha kujenga barabara ya mchepuko inayokwenda sanjari na ujenzi wa barabara mpya ya lami kutoka Songea hadi Lutukira kilometa 100.

“Kwa siku moja katika mji wa Songea malori 1000 yenye makaa ya mawe yanapita mjini Songea,barabara hii katikati ya mji wa Songea imekuwa kero na haiwezekani tena,tunaishukuru serikali kwa kutenga fedha mwaka huu ili kuanza ujenzi’’,alisema.

Naye Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wananchi wa Songea alipofanya ziara ya kikazi mkoani Ruvuma alisema amesafiri kwa njia ya barabara toka Dodoma hadi Songea na ameiona hiyo barabara ilivyochoka na kuchakaa hivyo serikali mwaka huu inaanza kujenga barabara hiyo kutoka Songea hadi Lutukira.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.